1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Wakutana tena kwa mazungumzo ya Kosovo

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUS

Viongozi wa Serbia na wa kabila la Waalbania walio wengi wa jimbo la Kosovo wanarudi tena Vienna leo hii kwa mazungumzo juu ya hatima ya jimbo hilo la Serbia lililojitenga.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Kosovo Agim Ceku tayari amesema kwamba hakuna cha maana cha kuzungumzia.Waalbania wa Kosovo wanadai uhuru baada ya kuwa chini ya himaya ya Umoja wa Mataifa kwa miaka minane.Waserbia wanasisitiza kwamba kamwe hawapaswi kupewa huru huo.

Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa Marti Ahtisaari alitaka kusitishwa kwa mazungumzo juu ya hatima ya jimbo hilo hapo mwezi wa Machi kwa kusema kwamba makubaliano kati ya Waserbia na Waalbania ni jambo lisilowezekana.

Ahtisaari alipendekeza jimbo la Kosovo lipatiwe uhuru chini ya usimamizi wa Umoja wa Ulaya lakini Urusi ilizuwiya kupitishwa kwa pendekezo hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.