VICTORIA: Rais wa China akamalisha ziara yake barani Afrika | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VICTORIA: Rais wa China akamalisha ziara yake barani Afrika

Rais Hu Jintao wa China amekamilisha ziara yake barani Afrika kwa kuitembelea Seychelles.Wakati wa ziara hiyo ya siku 12 rais Hu alizitembelea nchi 8 za Kiafrika.Hii ni ziara yake ya tatu barani Afrika tangu kushika madaraka mwaka 2003. Lengo kuu la ziara hiyo ilikuwa ni kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi na kisiasa pamoja na Afrika.Malighafi ya bara hilo inazidi kuwa na umuhimu kwa ukuaji wa kiuchumi wa China unaokwenda kwa kasi kubwa.Kabla ya Hu kuanza ziara yake,China ilitangaza kuwa itasamehe madeni ya nchi 33 za Kiafrika kama sehemu ya msaada wa Dola bilioni kadhaa ulioahidiwa mwaka jana kwa azma ya kusaidia kuchangamsha maendeleo barani Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com