VIANA DO CASTELO : Makubaliano ya mageuzi yako njiani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIANA DO CASTELO : Makubaliano ya mageuzi yako njiani

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana nchini Ureno hapo jana wamepuuzilia mbali shinikizo la Poland na kuapa kufikia makubaliano juu ya mageuzi ya umoja huo.

Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje Frank Walter Steinmeir muafaka unatazamiwa kufikiwa kabla ya kumalizika kwa kipindi cha urais wa Umoja wa Ulaya kinachoshikiliwa na Ureno mwishoni mwa mwaka huu.

Mazungumzo yalitiwa kiwingu na tafauti juu ya hatima ya jimbo la Kosovo na malalamiko ya Poland juu ya taratibu za kupiga kura na kupitisha maamuzi kwenye Umoja wa Ulaya.

Sio nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa kulipatia jimbo la Kosovo linalokaliwa na Waislamu wengi uhuru kutoka Serbia .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com