VATIKAN : Papa alaani umwagaji damu Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VATIKAN : Papa alaani umwagaji damu Gaza

Papa Benedikt wa 16 amelaani wimbi la hivi karibuni la umwagaji damu huko Gaza na amesema anahisi hususan yuko karibu na raia wanaoteseka kutokana na matokeo ya hali hiyo.

Akizungumza na watu wanaokwenda kuzuru na watalii katika Uwanja wa St.Peter kwa ajili ya sala yake ya baraka ya kila Jumapili pia ametowa wito kwa Israel na Wapalestina kurudi tena moja kwa moja katika mazungumzo ili kukomesha umwagaji damu.

Papa amesema kwamba viongozi wote wanapaswa kushirikiana kukomesha umwagaji damu huo kuongeza harakati za misaada ya kibinaadamu pamoja na kuunga mkono kuanza tena mara moja kwa mazungumzo ya moja kwa moja yalio makini na madhubuti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com