VATICAN: Afisa wa polisi ajiua | Habari za Ulimwengu | DW | 03.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VATICAN: Afisa wa polisi ajiua

Afisa wa polisi mjini Vatican Italia, amekufa kutokana na majeraha ya risasi katika tukio linalochukuliwa kuwa hatua ya afisa huyo kujiua mwenyewe.

Taarifa ya Vatican inasema afisa huyo mwenye umri wa miaka 25 alipatikana akiwa katika hali mbaya ndani ya bafu ya kambi yao mapema leo na kupelekwa hospitalini, ambako alikufa muda mfupi baadaye.

Wachunguzi wa Vatican wanachunguza ujumbe katika barua aliyowachwa na afisa huyo.

Tukio hilo limeleezwa kuwa baya kuwahi kutokea ndani ya makao ya Vatican tangu mwaka wa 1998 wakati afisa wa kikosi cha usalama cha Swiss Guard alipomuua kamanda wake na mke wa kamanda huyo kabla kujipiga risasi na kujiua.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com