Usanifu wa kuvutia nchini Ujerumani
Kila mwaka tuzo ya usanifu bora huwatambua wasanifu majengo waliopo ujerumani. Mwaka huu, hata hivyo, tuzo ya juu haikwenda tu katika jengo la kuvutia, lakini pia kwa jengo lililo na uhimilivu.
Kanisa la Emmanuel lililopo katika mji wa Cologne
Kanisa la Immanuel si kwamba ni ya kuvutia, lakini ni endelevu, na mtindo wake wa kisasa. Hii ni sababu iliyolifanya jopo katika tuzo ya wasanifu majengo ujerumani kuichagua kampuni ya Sauerbruch Hutton yenye makao yake mjini Berlin iliyobuni jengo hilo kuwa mshindi mkuu wa tuzo za mwaka 2015. Bonyeza katika link hii kuweza kuona majengo mengine ya kuvutia zaidi nchini Ujerumani.
Jengo la Lokdepot katika mji wa Berlin
Jengo la Lokdepot limesanifiwa na na kampuni ya ROBERTNEUN GmbH yenye makao yake mjini Berlin na kwa hakika ni jengo lililo zuri si tu kwa rangi yake. Dhana ya msanifu wa jengo hili ya "nyumba ya kiwanda" ilifanya majaji waweze kulichagua jengo hili katika tuzo za wasanifu majengo bora za mwaka 2015 iliyoshinda Euro 4,000.
Makumbusho ya Wayahudi katika mji wa Berlin
Mbunifu wa majengo wa Kimarekani Daniel Libeskind alikuwa mshindi wa tuzo wa wabunifu wa majengo nchini Ujerumani za mwaka 1999 baada ya kubuni jengo la makumbusho ya Wayahudi, jengo ambalo ni kubwa na la aina yake barani Ulaya. Umbo la mshazari la jengo hilo, linalotambulika kimataifa katika majarida ya wabunifu wa majengo ikiwa ni moja ya makumbusho bora.
Jengo la Kö-Bogen katika mji wa Dusseldorf
Libeskind amejenga majengo kadhaa ya kuvutia nchini Ujerumani. Mifano miwili ya majengo maarufu aliyoyajenga ni lile la Felix-Nussbaum House lililopo katika mji wa Osnabrück na jengo la kioo linalotumika kuwa makumbusho ya historia ya shirikisho la majeshi ya ujerumani lililopo katika mji wa Dresden. Mwaka 2014,Libeskind alizindua majengo ya Kö-Bogen katika mji wa Dusseldorf.
Ukumbi wa Elbe Philharmonic katika mji wa Hamburg
Huu ni ukumbi katika mji wa Hamburg unaotarajiwa kuwa ukumbi wa maonesho. Ukimbi huu umeanza ujenzi wake tangu mwaka 2007 Ni alama mpya katika mji huo. Kampuni maarufu ya usanifu wa majengo ya Uswiss ya Herzog & de Meuron ndio imehusika na ujenzi wake na limekuwa likizungumziwa sana , si kwasababu ya usanifu wake wa kuvutia bali kwasababu ya ongezeko kubwa la gharama za ujenzi wake.
Benki Kuu ya Ulaya katika mji wa Frankfurt
Makao makuu mapya ya Benki Kuu ya Ulaya katika mji wa Frankfurt ni majengo mawili yaliyo kama mnara yanayojitegemea. Majengo haya yamesanifiwa na kampuni ya Viennese architecture firm Coop Himmelb(l). Kampuni hiyo ilichaguliwa katika mashindano ya usanifu majengo ya kimataifa mwaka ya 2004. Ghorofa hii ndefu ni alama kubwa, ambayo huweza kutambulika kwa umbali wa upeo wa macho wa jiji hili.
Makumbusho ya Frieder Burda katika mji wa Baden-Baden
Mbunifu nyota Richard Meier amesanifu majengo kadhaa yaliyoshinda tuzo za makumbusho bora nchini Ujerumani. Makumbusho ya sanaa ya Baden-Baden yaliasisiwa na Frieder Burda ambaye alitaka kujenga nafasi ya maonyesho kwa kukusanya sanaa zake maarufu na kuzionesha. Makumbusho haya pia yamepokea tuzo za wabunifu bora za mwaka 2005.
Jengo la Kolumba katika mji wa Cologne
Msanifu majengo maarufu kutoka Uswiss Peter Zumthor ndiye aliyesanifu jengo lenye muundo wa kito katika mji wa Cologne, jengo la Kolumba ni makumbusho ya sanaa. Makumbusho haya hayana urembo wa kuvutia wala sehemu ya kunywa kahawa, hatahivyo ni moja ya vivutio vya watalii kutoka pande zote za dunia. Hii inatokana na mazingara yake tulivu katika mji huu wenye pilikapilika.
Ukumbi wa Hans Otto katika mji wa Potsdam
Tuzo ya usanifu wa jengo la ukumbi wa Hans Otto ilichukuliwa na Gottfried Böhm. Jengo hilo lililozinduliwa mwaka 2006, ni moja kati ya majengo yaliyo gumzo na moja kati ya kazi za mwishoni za tuzo za Pritzker, jengo hili pia limeelezwa kujengwa nae kuonesha mapenzi yake kwa marehemu mkewe ambaye alipenda rangi nyekundu.