Usain Bolt atamba tena katika mita 200 (19.19 sek.) | Michezo | DW | 21.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Usain Bolt atamba tena katika mita 200 (19.19 sek.)

Wakenya 13 wanaswa katika Lift Olympiic Stadium Berlin

default

Usain Bolt -mita 200

Bingwa wa mabingwa wa mbo za kas-Usain Bolt kutoka Jamaica, alifyatuka tena kwa kasi mno jana usiku na kunyakua medali yake ya pili ya dhahabu mara hii katika mita 200 na rekodii nyengine ya dunia ya sek. 19.19

Kikundi cha wakenya 13,kikiingiza mbunge John Pesa na mwenyekiti wa chama cha riadha cha Kenya ,Isaiah Kplagat chanasa nususaa nzima katka Lift ya uwanja wa Olimpk wa Berlin, jana .

Na Kongozi wa Tuimu ya wanariadha ya Afrika kusini,asema hatavumla tena kunyanyaswa kwa malkiia wao wa mta 800 Caster Semenya.

Baada ya medali yake ya plii ya dhahabu na rekodi nyengne ya dunia katika mita 200 ya sek.19.19 kutoka le ya zamanii ya sek.19.30, Usain Bolt jogoo la mashindano haya ya 12 ya Berlin, alinadi:

"Niliwaambia ninataka kuwa mwanariadha wa kukumbukwa maisha.Sifikiri kuweka rekodi.Sijiti shiindo.Najua la kufanya na nateremka uwanjani kutekeleza." Alisema nyota huyo wa Jamaica ambae jana alisherehekea siku yake ya kuzalwa kutimza miaka 22.

Mkasa wa msichana wa Afrika Kusin,alieshinda dhahabu katka mita 800 wanawake Caster Semenya, unaendelea kugonga vichwa vya habari.Semenya alkaribia jana kususia sherehe ya kumtunza medalii yake ya dhahabu na kupigiwa wiimbo wa tafa lake Afrika Kusni.

Na hvi ndivyo, mkuu wa Timu ya wanariadha wa Afrika kusini alivyokaripiia:"Sitaruhusu msichana huyu kunyanyaswa namna aliivyodhaliliwa.Hakufanya uhaliifu wowote.Uhalifu pekee aliotenda, nii kuzaliwa kama alivyozaliwa.Ametengwa kana kwamba ana maradhi ya ukoma-maradhi yatakayowadhuhuru hapa watu wengine."Alisema mkuu wa Timu ya wanariadha wa Afrika kusini huko Berlin.

Mkasa mwengine ulogonga vichwa vya habari jana uwanjani, ni kunasa kwa muda wa nusu-saa kwa kundi la wakenya katika Lifti ya uwanjani.Waheshiimiwa na vongozi wa riadha wa ujumbe wa Kenya 13 walikua ndani ya Lift kukagua iwapo wajenge kama hiyo katika Uwanja wa Kasarani,mjini Nairobi kwa mashindano ya mwakani 2010 ya riadha ya Afrika.Miongoni mwao alikuwa Prof.Saambli,mheshmiwa Nkaissery,kabanda wa Kabanda.Mbunge John Pesa na hata mwenyekiti wa chama cha riadha cha Kenya Isiah Kiplagat.

"Tuna wasi wasi mkubwa-subiriin-ni joto sana hapa -fungua mlango-mmekuwa mkituambia fundi anakuja tena mara 2-tuko watu 13-hatupati hewa ya kutosha-je mko Sauna ?"

Maji yalizidi unga jana uwanjani Berlin- je,wakenya watajenga Lift Kasarani ?

Muandishi:Ramadhan Alii

Mhari

 • Tarehe 21.08.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/JFnI
 • Tarehe 21.08.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/JFnI