Urusi kuwafidia wahanga wa shambulio la kigaidi
13 Aprili 2017Shambulizi hilo lilitokea katika shule moja kusini mwa mji wa Beslan. Katika taarifa kwa vyombo vya habari wizara ya ulinzi nchini humo imesema inaamini uamuzi huo wa mahakama ya Ulaya ya haki za binadamu iliko mjini Strasbourg haukuzingatia taarifa za kweli. Mahakama hiyo imeiagiza Urusi kulipa karibu Euro millioni 3 (Dola millioni 3.2)kufuatia kesi iliyowasilishwa na raia 409 wa Urusi ambao walionusurika shambulio au jamaa za waathirika.Mahakama hiyo ya haki za binadamu imesema maafisa wakuu nchini Urusi walikuwa wanafahamu kuhusu mipango ya shambulizi la kigaidi dhidi ya taasisi ya elimu katika eneo hilo ,lakini hakuna hatua za kutosha walizochukua kuilinda shule au kutoa tahadhari. Mahakama iligundua mapungufu chungu nzima kuhusu jinsi operesheni ya usalama ilivyoendeshwa.Matumizi ya vifaru, silaha zinazotumiwa kufyetua magurunedi na zana nyingine ulisababisha majeruhi miongoni mwa mateka.Wanamgambo waliokuwa na silaha nzito kutoka kusini mwa eneo la Caucasus nchini Urusi waliwakamata mateka zaidi ya watu 1,100 katika tukio lilochukua saa 50.Tukio hilo lilifanyika siku ya kwanza ya kufunguliwa shule Septemba mosi mwaka 2004. Zaidi ya watu 330 wakiwemo watoto 180 weliuawa na mamia ya wengine wakajeruhiwa. Kundi moja lililojitenga la wapiganaji wa kiislam lilikiri kuhusika katika shambulizi hilo. Kwa miongo kadhaa kumekuwepo na mashmabulizi yanayoendeshwa na wanagamabo wa kiislam huko Caucasus ambako ndiko iliko mji huo wa Beslan.
Mwandishi:Jane Nyingi/AFP/AP
Mhariri:Yusuf Saumu