Upatikanaji wa intaneti: mitandao ya kijamii, serikali na makampuni ya teknolojia
Huku Ujerumani ikijadili sheria ya mitandao ya kijamii ili kukabiliana na hotuba za chuki za mitandaoni, makampuni ya mitandao yameeleza hisia zao kuhusu namna itakavyowaathiri. Ni kwa kiasi gani? DW inaangazia.
Uhuru wa kujieleza ama maudhui yasiyoruhusiwa?
Iwe ni kauli za chuki, propanganda au uanaharakati, serikali za ulimwengu zimeongeza jitihada za kubana maudhui yanayofikiriwa kuwa ni kinyume cha sheria katika mitandao ya kijamii. Kuanzia kesi za mahakamani au marufuku za jumla, DW inachunguza jinsi nchi nyingine zinavyojaribu kuzuia ueneaji wa maudhui huku zingine zikijaribu kuwekea mipaka mitandao ya kijamii.
Sheria ya mitandao ya kijamii
Nchini Ujerumani waziri wa sheria Heiko Maas ametaka sheria itakayotoa faini kubwa kwa kampuni za mitandao ya kijamii kama Facebook, kwa kushindwa kuondoa taarifa zenye kauli za chuki. Lakini Facebook imepinga kwa kusema "kuzuia na kukabiliana na kauli hizo na habari bandia ni jukumu la jamii ambayo serikali haiwezi kuzuia". Sheria hiyo hivi sasa inapitiwa upya na kamati ya bunge al Ujerumani.
Haki ya kusahauliwa
Mwaka 2014, mahakama ya Ulaya iliamua kwamba raia wa Ulaya wana haki ya kuomba mtandao wa kupata taarifa kama Google and Bing, na kuondoa matokeo ambayo si sahihi, si muhimu ama yaliyozidi kwa kile walichoomba. Ingawa Google ililalamikia hatua hiyo, ilifanya hivyo kwa ukaidi, na kuonya kwamba inaweza kufanya upatikanaji wa internet kuwa huru zaidi ulimwenguni.
Zuio la jumla..
Mnamo mwezi May, Ukraineiliweka vikwazo dhidi ya Jukwaa la mitandao ya kijamii la Urusi pamoja na huduma zake za tovuti. zuio hillo la jumla liliwaathiri mamilioni ya Waukraine, wengi wao walikuwa na wasiwasi kuhusu taarifa zao. Hatua hiyo iliwasukuma vijana kuandamana mitaani, wakiitaka serikali kurejesha uwezekano wa kuingia kwenye majukwaa kama VKontakte (VK), ambalo ni kubwa zaidi Urusi.
Usafirishwaji wa taarifa binafsi
mwaka 2015, Mahakama ya Ulaya iliamua kwamba makubaliano ya miaka 15 ya "Safe Harbor" yaliyohusiana na usafirishwaji wa taarifa binafsi bila idhini ya kabla hayakuwa halali. Mwanafunzi wa sheria wa Kiaustria Max Schrems alianzisha mchakato wa kisheria dhidi ya Facebook kuhusiana na ufichuzi wa aliyekuwa mfanyakazi wa Usalama wa Taifa wa Marekani, NSA, Edward Snowden.
Kanuni
Nchini China, matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa yanaendeshwa na serikali. China imezuia kabisa upatikanaji wa maelfu ya majukwaa na tovuti, ambayo ni pamoja na Facebook, Twitter, Instagram na Pinterest. Na badala yake China inawapa wananchi wake uwezo wa kufungua mitandao ya kijamii ya ndani kama Weibo na WeChat, ambayo inatembelewa na maelfu kwa mamilioni ya watumiaji kwa mwezi.