1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Zaidi ya Wasudan 800 waliuwawa mwanzoni mwa mwezi huu Darfur

Saumu Mwasimba
12 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa na madaktari wa Sudan wamesema wanamgambo wa RSF na makundi ya wanamgambo wa kiarabu wamewauwa zaidi ya watu 800 katika mashambulizi waliyoyafanya katika mji mmoja ulioko katika jimbo la Darfur.

https://p.dw.com/p/4YiYZ
Baadhi ya wanajeshi wa Sudan wakiwa mjini Khartoum
Baadhi ya wanajeshi wa Sudan wakiwa mjini KhartoumPicha: AFP

Mashambulizi hayo dhidi ya mji wa Ardamata, ulioko katika mkoa wa Magharibi mwa Darfur yalifanyika mwanzoni mwa mwezi huu na ndiyo mashambulizi ya hivi karibuni kabisa katika msururu wa matukio ya mauaji katika jimbo hilo, kufuatia mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF.

Soma zaidi:UN: Nusu ya raia wa Sudan wanahitaji msaada wa kiutu

Sudan iko vitani tangu katikati ya mwezi Aprili baada ya mvutano kati ya mkuu wa majeshi, AbdelFatah al Burhani na jenerali Mohammed Hamdan Dagalo kugeuka kuwa mapambano kamili. Katika wiki za hivi karibuni kundi la RSF lilipiga hatua katika jimbo la Darfur na kuiteka kikamilifu miji yote mikubwa na vitongiji vyake, licha ya  kurudi kwenye meza ya mazungumzo ya kutafuta amani pamoja na jeshi nchini Saudi Arabia mwishoni mwa mwezi uliopita.