1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ununuaji wa bidhaa umeimarika.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVqN

Berlin.

Ununuaji wa bidhaa umeimarika nchini Ujerumani mwezi huu licha ya hali ya wasi wasi katika masoko ya fedha ya kimataifa.

Hata hivyo uchunguzi uliotolewa na taasisi ya utafutaji wa maoni GfK leo umeonya kuwa hali bora ya kiuchumi inaweza kuzuiwa kutokana na mfumuko wa bei.

Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni wa taasisi hiyo ya GfK kuhusu wanunuzi yanaonyesha ongezeko la moja ya kumi ya alama kuliko ilivyokuwa miezi miwili iliyopita. Ughali mkubwa wa maisha , udhaifu wa sarafu ya dola na shaka kuwa uchumi wa Marekani unaporomoka umepunguzwa na idadi ndogo ya wasio na kazi pamoja na uwezekano wa ongezeko la mishahara.