UNITED NATIONS:Baraza la Usalama la UN kupiga kura kuhusu Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 18.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

UNITED NATIONS:Baraza la Usalama la UN kupiga kura kuhusu Kosovo

Mataifa ya magharibi yanajiandaa kupiga kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuhusu mustakabal wa Kosovo huku Umoja wa Ulaya unaonya kuwa huenda ukaanzisha mazungumzo mapya pembezoni mwa yale ya Umoja wa mataifa.Urusi bado inapinga hatua ya kuipa Kosovo uhuru utakaosimamiwa na jamii ya kimataifa nyao mataifa ya Uingereza,Ufaransa na Marekani huenda wakawasilisha azimio lililoko tayari kupigiwa kura.

Nchi ya Urusi iliyo na kura ya turufu bado inaendelea kupinga azimio hilo linalotoa wito wa kufanywa mazungumzo kati ya makundi yanayofarakana ya Belgrade na Albania yaliyoko kwenye jimbo la Serbia.Mazungumzo hayo yanapaswa kuchukua muda wa siku 120.Urusi inakataa kuidhinisha hatua yoyote ambayo haikubaliwi na mwandani wake Serbia inayopinga vikali uhuru wa jimbo hilo lililo na raia wengi wa asili ya Albania.Urusi inachukulia jimbo hilo kama chimbuko la tamaduni na dini yake.

Kosovo imekuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka ’99 baada ya vita viliovyoendeshwa na NATO kuwafurusha majeshi ya Serbia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com