UN yapitisha azimio la vikwazo kwa Gaddafi
27 Februari 2011Matangazo
Azimio hilo linajumuisha kuzuia mali, marufuku ya kusafiri kwa Gaddafi na baadhi ya wanafamilia yake pamoja na kutekeleza vikwazo vya silaha.
Baraza hilo la usalama pia limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya The Hague, kuchunguza ukandamizaji uliofanywa dhidi ya raia wa Libya, uamuzi ambao umepokelewa na balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa, Peter Wittig.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa nchini Libya katika kipindi cha siku kumi zilizopita kutokana na ghasia.
Mwandishi:Grace Patricia Kabogo (RTRE,AFP,DPA)
Mhariri:Maryam Dodo Abdalla