UN yaidhinisha mapigano kusitishwa Gaza
9 Januari 2009Matangazo
Azimio hilo limepitishwa na nchi wanachama 14.Marekani imezuia kura yake.
Mswada wa azimio hilo uliopendekezwa na Uingereza na kuungwa mkono na Marekani na Ufaransa uliweza kupatikana baada ya kufanywa majadiliano marefu na makubaliano kupatikana kati ya wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu na za Magharibi.Haijulikani kwa umbali gani Israel na Hamas zitatimiza masharti ya makubaliano hayo.
Miswada mingine iliyopendekezwa hadi hivi sasa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza ilipingwa na Marekani na Uingereza.