1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMamlaka ya Palestina

UN: Wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa Gaza

20 Januari 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya wanawake UN Women limesema wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa katika vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4bUgS
Mwanamke raia wa Palestina akimkumbatia mwanawe katika hospitali ya Kuwait
Mwanamke raia wa Palestina akimkumbatia mwanawe katika hospitali ya KuwaitPicha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Shirika hilo limeeleza kuwa, wanawake na watoto 16,000 wameuawa na takriban akina mama wawili wanapoteza maisha yao kila baada ya saa moja. Limeongeza kuwa, wanawake wapatao 3,000 wamekuwa wajane na watoto 10,000 wamepoteza baba zao.

Katika ripoti iliyotolewa jana, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema wanawake na watoto ndio wanaokabiliwa na mzigo mkubwa katika vita hivyo na kulazimika kuhama mara kwa mara.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Sima Bahous amesema kuwa, kati ya wakaazi milioni 2.3 wa Gaza, watu milioni 1.9 wamepoteza makaazi yao huku karibu milioni moja wakiwa wanawake na watoto.