1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN waishutumu Sudan kwa kushambulia vikosi vyake

9 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/CmmC

KHARTOUM

Umoja wa mataifa umeishutumu serikali ya Sudan kwa kile Umoja huo ulichikitaja kuwa ni uvamizi dhidi ya ujumbe wake na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur. Umoja wa mataifa umesema dereva wake raia wa Sudan alijeruhiwa vibaya jumatatu usiku katika shambulio la kwanza dhidi ya jeshi la kusimamia amani la Umoja huo na Umoja wa Afrika.Duru kutoka eneo hilo zinasema wanajeshi wa Sudan walikishambulia kikosi hicho cha kuweka amani baada ya kudhania kuwa ni waasi.Lakini Umoja wa Mataifa amesema kwenye taarifa yake kwamba ujumbe wa wanajeshi wake umewekwa alama mahsusi kwa ajili ya usalama.