Umuhimu wa kutunza miti
Siku ya kiamataifa ya misitu ni wakati wa kuyafahamu mazingira yetu ya kijani. mwaka huu, inaangazia nishati mbadala, kwa wakati uliopita na sasa, na kuzungumzia nishati mbadala kongwe: Kuni.
Wito kwa ajili ya mbao
Misitu, mbao, vichaka, msitu mdogo, yote haya ni maeneo ya mapori yanayochukua ajenda kubwa katika siku ya kimataifa ya mistitu duniani Machi 21. Siku hii ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2012. Kila mwaka ikiwa na kauli mbiu tofauti tofauti na imejikita katika kuhamasisha misitu na matumizi mbalimbali. Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Misitu na Nishati".
Misitu kama chanzo cha nishati
Misitu ni chanzo cha aina nyingi za nishati. Ikitumiwa kama mafuta, mbao inaweza kuja katika aina tofauti ya fueli ngumu, gesi na kimiminika. Nishati ya mbao na mkaa, gesi ya mbao na mafuta ya kimiminika ama bio-ethani hutumika kama nishati kwa kaya moja kati ya tatu duniani. Hii inamaanisha watu milioni 2.4 duniani. Matumizi ya kawaida ya mafuta ya mbao majumbani ni pamoja na kupika na kutia joto
Mbao kama nishati mbadala
Misitu mizuri ya zamani na nishati inayozalisha ni ya kale lakini iliyo chanzo cha nishati endelevu . Inakadiriwa kufikia asilimia 40 ya nishati mbadala duniani kote. Tofauti na mafuta yaliyozalishwa kutokana na mabaki ya wanyama na mimea, uzalishaji wa hewa unaowekwa wazi angani wakati wa kuchoma mafuta ya mbao baadae hutolewa tena wakati miti inapopandwa, kwasababu inatumia na kuhifadhi C02.
Moshi husababisha mauti
Karibu asilimia 50 ya mbao inatumika kama nishati kila mwaka, zaidi ikichomwa kwa ajili ya mafuta. Kiwango hiki cha asilimia kilipanda na kufikia asilimia 60 huko Asia na asilimia 90 Afrika. Lakini Moshi unasababisha matatizo hususan kwa afya ya binadamu. Watu milioni 4.3 hufariki kila mwaka kwasababu ya uchafuzi wa hewa ya ndani. Hivyo ni vifo vingi zaidi ya vile vya Malaria, kifua kikuu na HIV
Kufanya kazi na mbao
Mbao ni chanzo muhimu cha ajira. Katika nchi zinazoendelea karibu watu milioni 883 hutumia maisha yao yote au sehemu ya maisha yao msituni. Kutokana na ukuaji wa uzalishaji mafuta , idadi hii inaweza kuongezeka, hata kwenye nchi zilizoendelea.
Kutoka Mbao za kung'olewa hadi taka ngumu za wanyama?
Umaarufu wa taka ngumu za wanyama na makaa umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Mwaka 2015, tani milioni 28 zilizalishwa. Sio tu kwamba ni nogo na nyepesi kushughulikia, pia zinaweza kuzalishwa kutoka akiba nyingine kama vile nyasi au taka. Faida nyingine ya nishati hii ukilinganisha na zile za kimiminika au gesi kutoka Fossil fuel, pellets ni salama katika usafirishaji.
Kivuli na ubaridi katika miji iliyo na joto
Je Mbao ni nzuri tu kwa kutia joto?Sio lazima. Kwa namna sayari inavyozidi ujoto, miti inaweza kutumika katika kuipooza. Katika miji ambayo ina joto kali , miti inaweza kupooza mazingira hadi nyuzi joto 8. Kwa matokeo hayo, miji iliyo na joto la chini inahitaji nishati kidogo kwa ajili ya hali ya hewa katika majengo. Hapa miti kufanya tena miujiza yake .
Kitisho cha mapafu ya kijani katika sayari
Misitu ya mvua inayo jukumu katika kuchota carbon dioxide (CO2). Misitu muhimu ya Amazon ipo chini ya kitisho kutokana na ukataji miti huku maeneo yakisafishwa kwa ajili ya kilimo, uchimbaji au miradi ya ujenzi. Wanasayansi wanaonya kwamba misitu hii ni lazima iokolewe ikiwa hali ya hewa duniania inahitajika kulindwa.