1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kimataifa ya Wanawake yaadhimishwa

Saumu Mwasimba
8 Machi 2019

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwa na fikra sawa, ujenzi bora kwa ajili ya ubunifu wa kimaendeleo wakati dunia ikiwa imetawaliwa na ubunifu,kujenga na kuleta mabadiliko ya jinsi watu wanavyoishi katika dunia.

https://p.dw.com/p/3EezG
Europäisches Parlament Weltfrauentag 2019
Picha: EP/V. Van Doornick

Ubunifu ndio kitu kikubwa kilichoishikilia duniani hivi sasa na kwa maana hiyo kuna haja ya kuona kwamba wanawake sio tu wanageuka kuwa wateja wa ubunifu huu lakini pia wachukue nafasi ya kuwa wabunifu wenyewe. Kwa kujihusisha kwao katika masuala yote ya ubunifu na kutafuta ufumbuzi ni mambo yanayoweza kuziangazia kwa njia ya kipkee haja au mahitaji ya wanawake na wasichana kutokana na kazi zao mpaka kwenye uzalishaji wa bidhaa,huduma na miundo mbinu kwa ajili ya wanawake wa matabaka mbali mbali.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kimataifa ya wanawake,fikiri kwa usawa,ujenzi bora na ubunifu kwa ajili ya mabadiliko ni kauli mbiu inayoliweka suala la ubinifu katika nafasi muhimu ya juhudi zinazoonesha haja na mitizamo ya wanawake pamoja na wasichana sambamba na kuyatatua masuala ambayo ni vizingiti katika huduma za umma na fursa.

Suala la kutofikiwa wanawake katika maeneo ya vijijini halipaswi tena kuwa sababu ya kuwatenga wakati ambapo kuna teknologia kama zile za kutoa na kufikisha fedha kwa njia ya simu na huduma ya kufanya malipo kwa njia za kidigitali, haya yakiwa ni mambo yanayoweza kuwa na faida kubwa za kijamii kwa hata wale wanaoishi vijijini kabisa.

Changamoto bado zinawakwamisha wanawake

Ukosefu wa barabara sio suala linalohitajika kuwa kizingiti cha kuzuia huduma za matibabu  kuyaokoa maisha ya wagonjwa,wakati ambapo kuna mbinu za ubunifu,mfano kama ile iliyogunduliwa na kijana wa miaka 15 wa Nigeria Eno Ekanem ya kutumika ndege zisizokuwa na rubani kudondosha vifurushi vya dawa katika maeneo ya vijijini kwa kudhibitiwa kwa njia za ujumbe mfupi wa sms.

Ghana Project BG Ghana's viele Gesichter
Picha: Imago/F. Stark

Ukosefu wa nguvu za umeme sio kizingiti tena kinachowafanya wanawake wasijifungue salama watoto wao katika maeneo ya vijijini. Mkunga Lorina Karway anasema katu hawezi kushindwa kuwasaidia kina mama wasijifungue salama usiku vijijini huko nchini Liberia kutokana na ukosefu wa nguvu za umeme,alichokifanya ni ubunifu.

Anatumia simu yake kupata mwanga wa kutosha kuwasaidia wajawazito kujifungua. Sio hilo tu lakini hivi sasa pia taa za gharama ndogo za kutumia umeme wa nguvu ya jua zinazotengenezwa na wanawake zimemfanya mkunga huyo kupata suluhisho endelevu katika kazi yake na vituo chungunzima vya afya vinatumia taa hizo na hata katika makaazi ya watu ambako awali walikosa huduma za umeme.

Juu ya hilo jukwaa maalum kwaajili ya wajasiriamali wanawake linalotumia teknolojia ya simu kuwaunganisha wakulima wanawake na kutowa taarifa za vyama vya ushirika,fedha na masoko ni huduma nyingine inayosaidia kutowa fursa kwa wanawake kupata soko.

Kuanzia Senegal barani Afrika mpaka Mashariki ya kati nchini Syria wanawake wameonesha juhudi kwamba hakuna kinachoshindikana. Msanifu majengo wakike kutoka Syria Marwa al Saboun alishinda tuzo kutokana na fikra yake ya unezi mpya wa mkoa wa Baba amr,huko homs ameonesha njia za kuweza kuzrudisha ushirikiano,mjongeleano na mwamko wa kujitambua baada ya vita hivyo vilivyoiharibu kabisa nchi yake.

(Umoja wa Mataifa)