1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yailenga meli ya kivita ya Urusi Bahari Nyeusi

26 Machi 2024

Jeshi la anga la Ukraine limesema limezidungua droni zote 12 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia Jumanne

https://p.dw.com/p/4e7kl
Ukatikaji wa umeme Kharkiv
Mashambulizi ya Urusi mjini Kharkiv yasababisha kukatika kwa umeme.Picha: Vyacheslav Madiyevskyy/Ukrinform/IMAGO

Katika taarifa, jeshi hilo limesema ndege hizo zisizokuwa na rubani zilizotengenezwa nchini Iran, zilidunguliwa kusini mwa miji ya Mykolaiv na Kharkiv.

Wakati hayo yakiarifiwa, msemaji wa jeshi la majini la Ukraine Dmytro Pletenchuk amesema leo kuwa Ukraine imeilenga meli ya kivita ya Olshansky ambayo Urusi iliiteka kutoka Ukraine mwaka 2014.

Ukraine | Vita | Mashambulizi ya Roketi dhidi ya Kyiv
Mashambulizi ya roketi mjini KyivPicha: Gleb Garanich/REUTERS

Urusi iliiteka meli hiyo pamoja na wanajeshi wa Ukraine wakati ilipoliteka eneo la Crimea mwaka 2014. Katika siku za hivi karibuni, Ukraine ambayo haina meli zozote kubwa, imefanikiwa kuzishambulia meli za Urusi katika Bahari Nyeusi kwa kutumia makombora au droni za majini.

Soma pia: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa ndege za droni

Wakati huo huo Rais Vladimir Putin wa Urusi amekiri kwamba shambulizi lililofanyika Jumatatu mjini Moscow katika tamasha la muziki lilifanywa na wanamgambo wa kiislamu ila akasema huenda ikawa Ukraine ilikuwa na dhima.

Ufaransa imeungana na Marekani kwa kusema kwamba ripoti za ujasusi zinaonesha kwamba lilikuwa shambulizi la wanamgambo.