Ujerumani na Ufaransa zapendekeza mabadiliko ya mkataba wa EU
6 Desemba 2011Viongozi hao wawili wamependekeza mabadiliko mapya katika mkataba wa ulaya, kwa lengo la kufanikisha lile linalokusudiwa mwishoni mwa Machi. Viongozi hao wamesema watawasilisha mipango yao kwa rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy hapo kesho ikiwa siku moja kabla ya mkutano mkubwa wa viongozi wote wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya unatoarajiwa kufanyika Brussels keshokutwa.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Paris baada ya mkutano wao wa muda mrefu, Merkel amesema wana nia ya uhakika kuiletea utulivu sarafu ya euro na kuimirisha ushindani katika kanda ya euro.
Pamoja na mambo mengine mkataba huo mpya utajumuisha vikwazo vya moja kwa moja kwa wanachama watakaokiuka kanuni.Kimsingi mkataba huo utaidhinishwa na nchi zote 27 za Umoja wa Ulaya lakini Sarkozy alisema saini za nchini 17 zinazotumia sarafu ya euro zitakubaliwa.