1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UINGEREZA YASISTIZA VIKWAZO VIWEKEWE ZIMBABWE.

Mwagodi, Isabella14 Julai 2008

Mzozo wa kuiwekea Zimbabwe vikwazo unazidi kupamba moto huku waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown,

https://p.dw.com/p/EcQ0
Waziri wa Uingereza,Gordon Brown.Picha: AP

Uingereza inatafuta kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya katika kuiwekewa Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi baada ya Urussi na China kukataa kutumia kura ya veto kupinga vikwazo dhidi ya Zimbabwe vikwazo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa Uingereza Gordon Brown aliwaambia waandishi habari katika mkutano wake wa kila mwezi," nimewauliza maafisa wa wizara ya fedha kushirikiana na tume ya kushughulikia migogoro ya kifedha, kufuatilia mali inayomilikiwa na utawala wa rais Mugabe ili tuweze kuchukua hatua mwafaka katika siku za hivi karibuni,"

Waziri mkuu huyo, amesema, ikiwa mazungumzo ya upatanishi hayatafua dafu Zimbabwe, Tutarudi kwenye kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Na matafia ya Russia na China yanayopinga vikwazo yatalazimika kukubali hatua ya vikwazo katika Umoja wa Mataifa''.

Lakini naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi , Sergei Kislyak,ailisema Urusi haikukiuka maazimio yeyote ya Umoja wa Ulaya kuhusu Zimbabwe kwani tayari walieleza msimamo wao wa kupinga vikwazo.

Urusi na China zilipinga Zimbabwe kuwekewa vikwazo katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuhoji kwamba Utawala wa rais Mugabe umeanza mazungumzo ya upatanishi na upande wa upinzani.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini Brussels kwa siku mbili wiki ijayo,na Brown amesema atawataka kuongezea majina ya wahusika na mashirika ya Zimbabwe watakayolenga katika orodha ya waonaolengwa kuwekewa vikwazo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband akiwa katika sherhe za kitaifa huko Paris,alisema atashinikiza hatua ya kuiwekea Zimbabwe vikwazo kwenye kikao hicho cha mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya. Hatua hiyo ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya hatahivyo itawalenga tuu maafisa wakuu 132 wa utawala wa rais Mugabe.

Lakini mshinid wa tuzo ya nobel Wangari Maathai aliwaambia waandishi habari jijini Nairobi kwamba wanashinikiza viongozi wa upinzani MDc na chama tawala cha Zanu-Pf kufanikisha mazungumzo ya upatanishi yalioanza wiki iliyopita na kupinga pedekezo la vikwazo,

``watakaoumia si viongozi bali wananchi,jukumu la amani ni lao viongozi

Tayari Chama tawala cha rais Mugabe na Upinzani walifanya kikao cha kwanza cha mazungumzo ya upatanishi wiki iliyopita. Mazungumzo hayo yanaongozwa na Morgan Tsvangirai wa upinzani maafisa wa Afrika kusini na wa chama tawala cha Zanu-Pf.

Viongozi wamekubali kutia saini mkataba wa maelewano wa mazungumzo ya upatanishi. Mkataba huo unatarajiwa kuweka mwongozo wa mazungumzo hayo yatakayofanyika kila baada ya siku 14.