Ugonvi wa ujasusi wapelekea vikwazo vya Rushia dhidi ya Georgia | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ugonvi wa ujasusi wapelekea vikwazo vya Rushia dhidi ya Georgia

Rushia imeweka vikwazo dhidi ya Georgia kufuatia kuachiliwa huru kwa maafisa wanne wa kijeshi wa Rushia waliyokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kutoa siri kuhusu mizozo iliyoko kati yake na majirani zake kutoka jamhuri za muungano wa Sovieti ya zamani. Moscow imetangaza vikwazo vya ndege, treni na posta dhidi ya Georgia licha ya wito wa Marekani na nchi za Ulaya ya magharibi wa kuisihi isifanye hivyo.

Kukamatwa na kuachiliwa huru kwa maafisa hao wa kijeshi wa Rushia nchini Georgia kumefuatia hali ya kutisha iliyokuweko kwa muda wa kutosha sasa kufuatia harakati za Georgia kujiunga na jumuiya ya kujihami ya nchi za kambi ya magharibi NATO na pia kujiunga na Umoja wa Ulaya wakati ambapo Rushia ingependelea kuendelea kuwa na ushawishi nchini Georgia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com