1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yangojea matokeo ya uchaguzi

P.Martin/ZPR/AFPE19 Februari 2011

Uchaguzi wa bunge na rais uliofanyika nchini Uganda siku ya ijumaa unatazamiwa kumrejesha madarakani Rais Yoweri Museveni kwa awamu ya nne.

https://p.dw.com/p/R2OB
President Yoweri Museveni of Uganda addresses a press conference at Naklasero State House, Kampala, Thursday, Sept. 29, 2005. Museveni threatened Thursday to send troops within the next two months to neighboring Congo to disarm scores of Ugandan rebels there if U.N. peacekeepers and Congo failed to disarm them. (AP Photo/ Michael Makutu )
Rais Yoweri Museveni wa UgandaPicha: AP

Kiasi ya watu milioni 14 walikuwa na haki ya kupiga kura.Lakini kampeni ya uchaguzi iliingia dosari kufuatia madai kuwa chama tawala kilinunua kura. Sasa zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa linaendelea huku Rais Museveni na mpinzani wake mkuu Kizza Besigye wa chama cha IPC, wakitabiri kuwa watashinda.Matokeo ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa siku ya Jumapili.