1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yashutumiwa kusaidia ukandamizaji wa al-Sissi

Sekione Kitojo
2 Julai 2018

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema Ufaransa imeshiriki katika ukandamizaji wa kinyama katika muda wa miaka mitano iliyopita kwa kuuza silaha na mifumo ya uchunguzi ya Rais Abdel Fattah al-Sissi. 

https://p.dw.com/p/30fZA
Ägypten Präsident Abdel Fattah al-Sisi
Picha: picture-alliance/dpa

Uchunguzi huo ulioidhinishwa na makundi manne ya haki za binadamu ya Ufaransa na Misri, uligundua kwamba mauzo ya silaha yameongezeka kutoka euro milioni 39.6 hadi bilioni 1.3 kati ya mwaka 2010 hadi  2016.

Wamedai kuwa makampuni ya Ufaransa ni washirika katika kile walichokiita, ukandamizaji usiokoma, tangu Sissi alipomuondoa madarakani rais mwenye anayefuata misimamo ya dini ya Kiislamu, Mohammed Mursi mwaka  2013. 

Ripoti hiyo imedokeza kuhusu makampuni yanayouza teknolojia inayotumika katika kuingilia kati data za mawasiliano ya umma na udhibiti wa makundi ya watu zinazotumiwa katika mfumo wa uchunguzi ambao mamia kwa maelfu ya wapinzani na wanaharakati wamekamatwa.