Ufaransa itaondosha wanajeshi wake maalum 200 kutoka Afghanistan. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ufaransa itaondosha wanajeshi wake maalum 200 kutoka Afghanistan.

Paris:

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa amesema nchi yake itaondosha mamia ya wanajeshi wake maalum kutoka Afghanistan. Michele Alliot-Marie alitoa tangazo hilo kwa waandishi wa habari alipoutembelea mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Wanajeshi maalum 200 wa Ufaransa wamewekwa Mashariki ya Afghanistan kama sehemu ya operesheni ya kupambana na ugaidi. Ufaransa imepeleka wanajeshi 2,000 hadi Afghanistan, waliobakia wamo ndani ya jeshi la kimataifa la usalama linaloongozwa na NATO. Hatua hiyo ya Ufaransa kutaka kuondosha wanajeshi wake maalum imekuaja katika wakati ambapo makamanda wa NATO wanataka wanajeshi zaidi wapelekwe Kusini mwa Afghanistan ambako wapiganaji wa Taliban waendesha harakati nyingi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com