1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Uefa Euro 2012; Ugiriki haina lake kwa Ujerumani

Ujerumani imefanikiwa kuingia katika nusu fainali ya mashindano ya kombe la mataifa ya ulaya Uefa , Euro 2012 kwa kuifungisha virago Ugiriki na kuweka miadi na ama Uingereza ama Italia.

(L-R) UEFA President Michel Platini, German Chancellor Angela Merkel, president of the German soccer federation (DFB) Wolfgang Niersbach and German Interior Minister Hans-Peter Friedrich react after a goal that was disallowed during the quarter-final soccer match between Germany and Greece at the PGE Arena in Gdansk, June 22, 2012. REUTERS/Peter Andrews (POLAND - Tags: SPORT SOCCER POLITICS)

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akishangiria bao la Ujerumani

Gazeti moja liliandika nchini Ujerumani , na hapa nanukuu, "samahani Ugiriki, kwa hili hatuwezi kuwaokoa". Ni maneno yanayolenga kuifahamisha Ugiriki kuwa katika soka hakuna mpango wa kuiokoa kama uliotolewa na mataifa ya eneo la euro wa kuiokoa nchi hiyo kiuchumi.

Kikosi cha Ujerumani kiliiendesha puta Ugiriki na hatimaye kuibwaga kwa mabao 4-2 na kuwa timu ya pili kufanikiwa kuingia katika nusu fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2012, Ijumaa (22.06.2012) katika mchezo ambao ulikuwa karibu wa upande mmoja na ambao ulipewa vionjo vingine zaidi kutokana na mvutano wa kisiasa na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.

Greece's Giorgos Tzavellas reacts after Germany scored the opening goal during their Euro 2012 quarter-final soccer match at the PGE Arena in Gdansk, June 22, 2012. REUTERS/Bartosz Jankowski (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)

Maji yamezidi unga kwa Ugiriki.

Kansela ashuhudia pambano

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa uwanjani kushuhudia pambano hilo, mtu ambaye anachukiwa nchini Ugiriki kwa kuonekana kuwa ndie anayelazimisha masharti magumu ya kubana matumizi ili kupata mkopo wa kuiokoa kiuchumi , kikosi hicho cha Joachim Loew kilipata ushindi rahisi mwishoni na kitakwaana na Uingereza ama Italia katika pambano la nusu fainali.

Ugiriki , ikitumai kurudia kile ilichokifanya mwaka 2004 katika mashindano ya kuwania kombe hili, ilianza kwa kulinda lango lao kwa nguvu zote katika nusu ya kwanza ya mchezo, lakini walifungashwa virago kwa mapigo yaliyonyooka ya washambuliaji wa Ujerumani , huku Merkel akishangiria.

Wagiriki wavunjika moyo

Tulitaka kushinda kwa hali yoyote ile, na ingekuwa inashangaza kwa watu nyumbani Ugiriki, amesema shabiki mmoja wa Ugiriki anayeishi mjini Zurich Aliks Fotiou, na ambaye amekwenda Poland na dada yake na watoto wake wawili wa kike kushuhudia pambano hilo.

Tumepata mabao mawili na haya yanatupa faraja. Tumejaribu kwa nguvu zetu zote lakini Wajerumani ni timu ngumu sana.

Ndio kulikuwa na hii hali ya shauku kabla ya mchezo, lakini nafikiri mashabiki wote kutoka Ugiriki na Ujerumani na Poland wamesaidia kuifanya hali kuwa ya furaha, ya urafiki na tamasha la soka, amesema shabiki wa Ujerumani Joerg Himmler, ambaye amesafiri saa 20 kwa treni kutoka Heidelberg hadi Gdansk, kwa ajili ya pambano hilo.

Kocha ataka kahawa

Lakini wakati nafasi baada ya nafasi zikipotea katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kocha wa Ujerumani Joachim Loew alikuwa na wasi wasi ambapo nusura aondoke kwenda katika vyumba vya kuvalia ili kupata kahawa.

Germany's coach Joachim Loew (R) and Greece's coach Fernando Santos react during their Euro 2012 quarter-final soccer match at the PGE Arena in Gdansk, June 22, 2012. REUTERS/Thomas Bohlen (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)

Kocha wa Ujerumani Joachim Loew

Hatimaye mambo yalikuwa mazuri kwa Ujerumani , na kikosi cha Joachim Loew kiliingia katika nusu fainali ya mashindano haya. Nilijaribu kwenda kupata kikombe cha kahawa lakini tukakosa nafasi nyingine na nilikasirika sana, amesema Joachim Loew mwenye umri wa miaka 52, ambaye anafahamika kwa mapenzi yake ya kahawa.

Wakati Ugiriki iking'ang'ania sare ya bila kwa bila , Marco Reus alipata nafasi na kupiga mpira nje na Loew karibu apate wazimu. Loew aliamua kucheza kamari kwa kufanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kumuacha nje Mario Gomez na kuamua acheze Miroslav Klose na kumuacha Thomas Mueller na Lukas Podolski katika juhudi za kuwachanganya Wagiriki.

Germany's Philipp Lahm (L) and Marco Reus celebrate after Lahm scored a goal during the Euro 2012 quarter-final soccer match against Greece at the PGE Arena in Gdansk, June 22, 2012. REUTERS/Kai Pfaffenbach (POLAND - Tags: SPORT SOCCER TPX IMAGES OF THE DAY)

Nahodha wa Ujerumani Phillip Lahm baada ya kufungua mpango wa Ugiriki

Ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa lakini licha ya kuchukua dakika 39 kuanza kufungua milango ya Ugiriki, kwa goli la nahodha Phillip Lahm , ilidhihirisha kuwa ni uamuzi sahihi.

Uhispania watatetea taji lao?

Jumamosi (23.06.2012) ni siku ya tatu ya awamu ya robo fainali wakati Ufaransa inakwaana na Uhispania, mjini Donetsk, nchini Ukraine , kabla ya hapo Jumapili (24.06.2012) ambapo Uingereza inamiadi na Italia mjini Kiev.

Mwandishi : Sekione Kitojo/ rtre