1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Udugu wa Kiislam wadai kushinda Misri

Chama cha Udugu wa Kiislam nchini Misri kimedai kuwa mgombea wake Mohammed Mursi anaongoza katika matokeo yaliokwisha hesabiwa kufuatiwa uchaguzi uliomalizika hivi karibuni.

v l n r: Ahmed Shafik, Hamdeen Sabahi, Amr Moussa, Mohamed Mursi, Abdel Moneim Abol Fotouh

Die fünf aussichtsreichsten Kandidaten der Präsidentschaftswahlen in Ägypten

Matokeo hayo ambayo yamebandikwa katika mtandao wa chama hicho, yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Hosni Mubarak Ahmed Shafique anashika nafasi ya pili lakini msemaji wake hakuweza  kuthibitisha madai hayo. Matokeo rasmi yanatarajiwa kuanzia siku ya Jumapili. Kama mambo yataendelea kama yalivyo,  wawili hao watapambana katika duru ya pili itakayofanyika tarehe 16 na 17 mwezi ujao.

Chama cha udugu wa Kiislam kilisema Mursi alikuwa ameshakusanya theluthi moja ya kura, akifuatiwa na Shafique aliyepata asilimia 22. Msoshalisti Hamdeen Sabbahi yuko katika nafasi ya tatu akiwa na asilimia 20 akifuatiwa na Abdul Moneim Abul Futouh mwenye asilimia 17 kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali yaliotolewa na chama hicho cha Kiislam.

Mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam Mohamed Mursi.

Mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam Mohamed Mursi.

Mursi mwenye umri wa miaka 60 na mwenye taaluma ya uhandisi aliingia katika kinyanganyiro hicho wiki tano zilizopita huku wapinzani wake wakimkejeli kwa kumuita tairi la akiba baada ya mgombea wa chama hicho wa awali kuondolewa na tume ya uchaguzi.

Uhusiano kati ya Misri na Israel na mapambano dhidi ya rushwa
Katika kampeni zake, Mursi alikuwa akiahidi kuweka utawala wa sheria nchini Misri na amekuwa akiweka wazi kuwa anataka kutizama upya mkataba wa amani kati ya Misri na Israel, akisema kuwa nchi hiyo jirani na Misri haija heshimu Mkataba huo. Lakini chama hiki kimesema hakitauvunja Mkataba huo.

Mursi pia aliahidi kupambana na rushwa iliyokithiri kutoka enzi za Mubarak na kupunguza ukubwa wa serikali. Katika kampeni zake, Mursi alitembea Misri nzima akitangaza ilani ya chama chake iliyotengezwa kwa misingi ya Uislam. Mafanikio yake yamewafadhaisha wasiyo egemea dini na wakristu ambao wana wasiwasi na ahadi yake kuwa watakuwa na uhuru wao chini ya utawala wa chama hicho.

Utawala wa sharia
Mohammed alisema katika kampeni zake mateso waliyokuwa wakiyapata Wamisri chini ya utawala wa Hosni Mubarak ni kwa ajili ya sheria za Kiislam na kwamba damu yao na kuishi kwao kunategemea utekelezaji wa azma hiyo, na kuongeza kuwa kwa pamoja watapigana kutekeleza azma hiyo.

Ahmed Shafiq anayeshika nafasi ya pili.

Ahmed Shafiq anayeshika nafasi ya pili.

Nyota njema kwa Dk. Mursi ilianza siku ya Jumatatu baada ya matokeo ya Wamisri waishio nje kumchagua kwa asilimila 49 licha ya kura za maoni zilizokuwa zkiendeshwa na mashirika yanayoegeme upande wa serikali yakimuweka katika nafasi za chini kabisaa.

Mursi ambaye alipata Shahada yake ya uzamivu nchini Marekani na ambaye alitumikia sehemu ya maisha yake jela chini ya uatwala wa Hosni Mubarak, ni kiongozi muandamizi wa chama cha Udugu wa Kiislam ambacho pia kilishinda zaidi ya nusu ya viti vya Ubunge.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga\RTRE\AFPE\DPAE
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman