1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Urusi wakosolewa.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJy

Moscow. Wachunguzi wa uchaguzi kutoka nje wamekosoa uchaguzi wa bunge nchini Urusi ambao chama cha rais Vladimir Putin cha United Russia kimeshinda na kusema haukuwa wa haki. Shirika la usalama na ushirikiano katika bara la Ulaya OSCE, na baraza la Ulaya yametoa matamshi hayo katika taarifa ya pamoja. Wakati kura zote zimekwisha hesabiwa , chama cha rais Putin cha United Russia kimepata theluthi mbili ya wingi wa kura katika uchaguzi huo uliofanyika jana Jumapili.Baada ya matokeo hayo rais Putin amesema kuwa wananchi wameweza kuamua ni chama gani wanachokihitaji.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Urusi, wakosoaji wa serikali na upande wa upinzani wameilaumu serikali kwa wizi wa kura na kutumia mbinu za kuwakandamiza wapinzani. Chama cha United Russia pamoja na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo vimepuuzia shutuma hizo na kusema ni za kizembe.