Uchaguzi wa duru ya pili umefanyika Zimbabwe | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Uchaguzi wa duru ya pili umefanyika Zimbabwe

Tsvangirai asema ni batili

default

Rais Mugabe wa Zimbabwe katika mkutano wake wa mwisho wa kampeini kabla ya upigaji kura wa leo Ijumaa

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe imefanyika, licha ya miito ya awali kutoka sehemu mbalimbali za dunia ya kutaka uahirishwe kutokana na kujiondoa kwa mmoja wa wagombeaji wa kiti hicho wa upande wa upinzani.

Ingawa umefanyika lakini pia umelaaniwa na jumuia ya kimataifa na kuuita dang'anya toto.

Kwa mara nyingine tena rais Mugabe ameipuuza jamii ya kimataifa akaendelea na uchaguzi wa urais wa duru ya pili.Miito ilisikika kutoka pembe mbalimbali za dunia zikitika uahirishwe.

Taarifa chache zilizotufikia kutoka Zimbabwe Ijumaa asubuhi zinaonyesha kuwa ni idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza.Haijulikani ikiwa ni sababu za kususia au vingine.

Mapema kiongozi wa upinzani Morgen Tsvangirai aliejiondoa siku sita zilizopita,akisema kutokana na ghasia na vitosho,anasema kuwa uchaguzi huo ni danganya toto na hautatambuliwa na ulimwengu.

Na kuongeza kuwa uchaguzi wa leo ni tendo la dikiteta anaetaptapa.Pia amesema kuwa wapiga kura wamepewa vitisho.

Mugabe mwenyewe amepiga kura katika mtaa wa Highfield Township nje ya mji mkuu wa Harare akiandamana na mkewe.Baada ya kupiga kura alipouliuzwa na waandishi habari anajisikiaje alijibu kuwa yuko sawa na matumaini.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilinukuliwa kusema kuwa uchaguzi ulikuwa unakwenda vizuri.

Uchaguzi huo umekosolewa ndani na nje ya nchi.Mawaziri wa nje wa mataifa ya Afrika wameijadili Zimbabwe kabla ya mkutano wa kilele utakaofanyika katika eneo la Sharm el-Sheikh nchini Misri.

Waziri mmoja ambae hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la Reuters, kuwa ,kwa maoni yake hawatayatambua matokeo ya uchaguzi huo ingawa walikuwa baado wanalijadili suala hilo.

Lakini Mugabe alivyo mkaidi amesema kuwa atahudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika na kukabiliana na wapinzani wake.

Kamati ya kiusalama ya jumuia ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC mapema wiki hii ilitaka uchaguzi wa Ijumaa uahirishwe,ikitoa hoja kuwa kuchaguliwa tena kwa Mugabe hakutakuwa na uhalali.Kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC Morgen Tsvangirai amesema anaamini kuwa yeye rais wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki atamtambua Mugabe baada ya uchaguzi wa leo.

Baada ya mkutano wa mataifa tajiri dunia ya G8 nchini Japan,waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,Bi Condoleezza Rice,amesema kuwa serikali yake itapendekeza suala la vikwazo zaidi dhidi ya Zimbabwe katika kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa huenda Mugabe anafanya hivyo ili kuweza kujiimarisha endapo atashurutishwa kujadiliana na Tsvangirai.

Mugabe anasema yuko radhi kujadiliana na MDC lakini kwa masharti ya kutoshinikizwa na mataifa ya kigeni

Tsvangirai, aliekuwa katika ubalozi wa uholanzi mjini Harare kwa mda, amesema leo Ijumaa

akiwa nyumbani kwake mjini Harare kuwa, uwezekano wa majadiliano upo japo unatatizwa na uchaguzi wa Ijumaa

anaosema si halali.

Aidha amewaomba viongozi wa kiafrika kuongoza majadiliano ili kusaidia raia wa Zimbabwe kuunda serikali ya mseto ambayo ni ya mpito.

Hata hivyo akasema kuwa mazungumzo hayo sasa yanatatizwa na uchaguzi aliouita batili.

Wasimamizi kutoka nchi za magharibi ambazo zinamkosoa sana Mugabe walipigwa marufuku nchini humo pamoja na waandishi wa habari wengi wa kigeni waliotaka kuripoti juu ya uchaguzi huo.

 • Tarehe 27.06.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/ES7e
 • Tarehe 27.06.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/ES7e

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com