1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge nchini Marekani

Saumu Ramadhani Yusuf3 Novemba 2010

Chama cha Republican cha shinda katika baraza la wawakilishi kwenye uchaguzi wa bunge na magavana

https://p.dw.com/p/Px3b
Rais Barack Obama na chama chake wapata kipigo katika uchaguzi wa bungePicha: AP

Chama cha upinzani cha Republican kimepata ushindi katika baraza la wawakilisha hali ambayo imeonekana na kipigo kwa rais Barack Obama.Chama hicho kimejinyakulia viti 58 mpaka sasa na kuonekana kuongoza katika maeneo mengine manane zaidi.Viti hivyo ni vingi zaidi kuliko walivyohitaji kuvidhibiti ambavyo ni 40.Ingawa chama cha Demokratic cha rais Barack Obama kimepoteza viti katika baraza hilo la wawakilishi wamenyakua ushindi katika majimbo muhimu kabisa kama vile Carlifornia.

Uchaguzi huo wa bunge na magavana nchini Marekani umeonekana kutawaliwa na rangi nyekundu rangi ambayo ni alama ya chama cha upinzani cha Republican.hali ambayo ilikluwa ikitarajiwa tangu hapo katika ulingo wa kisiasa.Hata kituo cha Matangazo cha Marekani cha CNN kilikuwa kimeshajiandaa kuwatangaza wahafidhina kuwa washindi ambapo dakika chache baada ya saa tatu ilikuwa imeshafahamika kwamba Republican wamepata wingi wa viti katika baraza la wawakilishi nchini humo.

John Boehner, kutoka chama hicho cha Republicana ambaye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya spika wa bunge baadae kufuatia ushindi huo wa chama chake alikuwa yuko tayari kabisa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi huo akisema.

'' Wamarekani wamemtolea ujumbe usikuwa na shaka kabisa leo hii,na ujumbe huo unasema badilisha mwelekeo''

Aidha hakusita kuzungumzia jinsi chama cha Republican kitakavyoigeuza hali ya mambo nchini Marekani na kufanya kazi kwa pamoja na rais Obama.

''ushindi wetu mpya kazi tofauti na ilivyokuwa .Tutachukua mwelekeo mpya ambao haujawahi kuchukuliwa na chama chochote tutapunguza matumizi badala ya kuyaongeza''

John Boehner anatazamiwa kuchukua mahala pa Nancy Pelosi katika bunge la Marekani''

Chama cha Republican sio tu kimenyakua ushindi mkubwa katika baraza la wawakilishi bali pia limepishana kwa kiasi kidogo sana na ushindi wa chama cha Demokrativc katika baraza la Seneti,kilikosa viti 10 pekee ili kichukue pia ushindi katika baraza hilo la Seneti.Kufikia leo asubuhi chama cha Demokratic kilikuwa kimepata viti 51 huku Republicans wakijinyakulia viti 46 huku kinyang'anyiro kikiwa kigumu katika majimbo ya Alaska,Colorado na Washington.

USA / Boehner / Kongresswahlen
John Boehner kutoka chama cha Republican atachukuwa nafasi ya spika wa bungePicha: AP

Kiongozi wa waliowengi katika baraza la Seneti kutoka chama cha Demokratic Harry Reid alifanikiwa kubakia katika kiti chake baada ya kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wake Sharron Angle.Ushindi huo wa Reid ndio uliowafanya wademokrats kuponea chupuchupu kupoteza wingi wao katika baraza la Seneti.Kinyang'anyiro katika jimbo hilo la Nevada pia kilikuwa cha aina yake kama alivyokiri mwenyewe Harry Reid aliyeshinda kwa asilimia 50 dhidi ya 45 za mpinzani wake-

''Nimeshashuhudia mapambano makali katika maisha yangu tangu mitaani,halafu kwenye uwanja wa ndondi na kisha katika baraza la seneti la Marekani.Lakini lazima nikiri kwamba haya yalikuwa ndio mapambano makali zaidi''

Aidha katika majimbo muhimu kama vile Carlifornia warepublican wameshindwa kuwashawishi wapiga kura ambapo Mdemokrat Barbara Boxer alifanikiwa kutwaa kiti chake kwa mara nyingine huku Jerry Brown pia wademokratic akinyakua kile cha ugavana na kuchukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Arnold Schwarzenneger.Jerry Brown alikuwa na kibarua kigumu cha kupambana na bwenyenye anayemiliki kampuni kubwa ya kunadi vitu katika mtanadao ya Ebay Meg Whitman.

Mwandishi Christina Bergman ZR/Saumu Mwasimba

Mhariri Josephat Charo