1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Abdu Said Mtullya26 Novemba 2011

Mikutano ya hadhara yapigwa marufuku mjini Kinshasa

https://p.dw.com/p/13Hmk
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoPicha: AP

Mkuu wa polisi katika mji wa Kinshasa amepiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya kampeni za uchaguzi baada ya mtu mmoja kufariki. Polisi pia walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa upande wa upinzani mnamo siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi hii leo.

Mkuu wa Polisi ya Kinshasa Jean de Dieu Oleko amesema mtu mmoja amepigwa jiwe kichwani karibu na uwanja wa ndege ambako maelfu wamekusanyika kuwasikiliza washindani wakuu wa uchaguzi wa jumatatu-Rais Joseph Kabila anaewania muhula mwingine na mwanasiasa mkongwe Etienne Tchisekedi.

Polisi inachunguza ripoti kwamba mtu mwengine ameuawa.Hali ilianza kuwa tete tangu jana baada ya kambi zote mbili-ile ya Kabila na yaTchisekedi kusema zinapanga kuitisha mikutano ya mwisho katika uwanja mkubwa kabisa wa michezo-Uwanja wa Mashahidi.