1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Marekani nchini Serbia watiwa moto

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBSL

BELGRADE:

Marekani imelaani mashambulizi ya ubalozi wake katika mji mkuu wa Serbia Belgrade.Magenge ya wafanya ghasia walitia moto jengo la ubalozi wa Marekani, wakipinga uhuru wa Kosovo.Maafisa wa Kimarekani wamesema maiti moja iliyoungua kabisa imekutikana ubalozini.Yasemekana,maiti hiyo ni ya mfanya maandamano kwani hakuna mfanyakazi wa ubalozini anaekosekana.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani mjini Berlin pia imesema,ubalozi wake mjini Belgrade umeshambuliwa na kumetokea hasara ya mali.Vikosi vya polisi wa Serbia vilivyosita hapo mwanzoni,baadae vilitumia gesi ya kutoa machozi kuyatawanya makundi ya wafanya ghasia.Kwa mujibu wa maafisa wa hospitali,watu 97 wamejeruhiwa ikiwa ni pamoja na polisi 32.Hapo awali Waziri Mkuu wa Serbia,Vojislav Kostunica alipohotubia zaidi ya watu 100,000 mjini Belgrade alisema,Kosovo daima itabakia sehemu ya Serbia.