Uandikishwaji wa upigaji Kura visiwani Zanzibar
7 Julai 2009Matangazo
Chama cha upinzani cha CUF kimelalamika kwamba kuna watu huko Kisiwani Pemba wananyimwa nafasi ya kujiandikisha, lakini maafisa wanaosimamia zoezi hilo wanasema hao walionyimwa nafasi hiyo hawajatimiza masharti yaliowekwa na sheria.
Othman Mirají alizungumza na mwandishi wa habari, Munir Zakaria, aliyoko sasa huko Konde, Pemba, ili anipe maelezo zaidi...