1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tvangirai asema mazungumzo ya kugawana madaraka yapiga hatua

Saumu Mwasimba17 Agosti 2008

Suali bado ni je nani atakubali kumuachia mwenzake aongoze nchi?

https://p.dw.com/p/Eyq2
Morgan Tvangirai na Robert Mugabe wavutana nani awe kiongozi wa nchiPicha: AP

Kiongozi wa chama cha Upinzani cha MDC nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai hii leo amesema kwamba mazungumzo juu ya suala la kugawana madaraka yamepiga hatua nzuri na kutoa matumaini huenda mzozo wa kisiasa nchini humo ukafikia kikomo.Tsvangirai ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa kilele wa viongozi wa eneo hilo.

Aidha chama cha MDC kitakutana viongozi wa nchi za kusini mwa Afrika katika mkutano huo kujaribu kuumaliza mvutano unaokwamisha juhudi za kuuokoa uchumi wa nchi hiyo uliosambaratika.

Hadi sasa Tsvangirai na rais Mugabe wanavutana juu ya nani atakuwa kiongozi wa nchi.Viongozi 14 wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC walijadiliana muswaada wa makubaliano ya kugawana madaraka katika kikao cha faragha ambacho pia kilihudhuriwa na rais Mugabe na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.

Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia zilizo karibu na kikao hicho ni kwamba makubaliano ya kugawana madaraka huenda huenda yakasainiwa hivi karibuni.Hapo jana rais wa Afrika Kusini ambaye amepewa jukumu la upatanishi katika mgogoro wa Zimbabwe amesema huu ni wakati muafaka wa kuunga mkono Mazungumzo hayo.