Tuzo ya Mo-Ibrahim
19 Oktoba 2009Matangazo
Taasisi ya Mo Ibrahim imeshindwa kumpata mshindi wa tuzo ambayo huwatunza viongozi bora wa Afrika
waliomaliza muda wao madarakani kwa kutoa mfano juu ya
demokrasia na utawala bora, imeshindwa kumpata mshindi wa tuzo
hiyo ya dola milioni 5 kwa mwaka huu wa 2009. Mmoja kati ya
wajumbe wa jopo la waamuzi ni Waziri Mkuu wa zamani wa
Tanzania, Dr Salim Ahmed Salim. Mohamed
AbdulRahman alizungumza naye kwa simu kutoka London
na kwanza alimuuliza sababu za taasisi hiyo kushindwa kumpata
mshindi mwaka huu .
Mtayarishaji: Mohammed Abdulrahman
Mhariri: Josephat Charo