TUNIS: Mke wa Arafat apokonywa uraia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TUNIS: Mke wa Arafat apokonywa uraia

Tunisia imempokonya uraia mke wa kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat. Suha Arafat, mwenye umri wa miaka 44, alizaliwa mjini Jerusalem na kuwa raia wa Tunisia mwaka jana.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa na wala kesi ya msichana wa Arafat wa umri wa miaka 12, Zahwa, ambaye alipata uraia wa Tunisia siku moja na mamake, haikutajwa.

Inaaminiwa Suha Arafat ameondoka Tunisia na ripoti zinaashiria yuko nchini Malta. Aliishi Tunisia tangu kifo cha mumewe mnamo mwezi Novemba mwaka wa 2004.

Suha alikataa kusema lolote alipohijiwa na gazeti la Al Hayat lililo na makao yake mjini London, Uingereza, akiwa mjini Valleta, ambako kakake, Ghabi Al Taweel, anafanya kazi kama balozi wa Palestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com