1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya uchaguzi Tanzania yatangaza rasmi taratibu za uchaguzi leo

16 Agosti 2010

Wajibu wa waangalizi wa uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huu umeangaziwa pia kwenye mkutano wa tume ya uchaguzi na waandishi habari jijini Dar es Salaam hii leo

https://p.dw.com/p/OoXq

Nchini Tanzania, maandalizi ya uchaguzi mkuu yameingia awamu nyengine wakati kampeni zitaanza tarehe 20 mwezi huu. Hii leo Tume ya Uchaguzi ya Tanzania, NEC imezitangaza rasmi taratibu za shughuli nzima pamoja na wajibu wa waangalizi wa uchaguzi. Uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Wagombea wa wabunge wa vyama kadhaa nao pia wanaendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu. Mwandishi wetu wa Dar es Salaam George Njogopa aliyehudhuria mkutano wa Tume ya Uchaguzi na ametutumia taarifa ifuatayo.