1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya maendeleo ya Afrika

19 Desemba 2007

Katibu mkuu wa zamani wa UM Kofi Annan amempongeza Kanzela Angela Merkel na Ujerumani kwa mchango wao katika juhudi za kulifufua bara la Afrika kiuchumi.

https://p.dw.com/p/CdbV

Kwa muujibu wa katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, uchumi wa bara la Afrika umeanza kukua na katika nchi nyingi za Afrika kuna matumaini mema ya kiuchumi. „Tukubali kwamba Afrika ndio inaanza kutambaa kiuchumi.“ alisema mjini Berlin jana mwenyekiti huyo wa Tume ya Maendeleo ya Afrika wakati wa mkutano wake mjini Berlin na Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani pamoja na wajumbe wengine wa Tume hiyo.

Barani Afrika hivi sasa kuna wachezaji wapya uwanjani nao ni China na India.Kwahivyo, hivi sasa ni jinsi gani wafadhili wa zamani na wapya watashirikiana na bara la afrika linalonyanyukia kiuchumi.

Hapa zinazofaa kuhesabiwa ni zile ahadi tu ambazo zaweza kutimizwa.Kwa upande wao nchi za kiafrika zinapaswa nazo kuimarisha mchango wao katika vita vya kupambana na rushua na utawala bora.

Katika swali hili, Kofi annan alipongeza mchango unaotolewa na Ujerumani na Kanzela wake Angela Merkel.Alisema:

„Kanzela amekuwa akitusaidia sana.Nadhani naweza leo kusema yeye ni miongoni mwa mabingwa katika juhudi za Afrika kutekeleza shabaha za milenium.Alizuru Afrika binafsi kujionea hali ya mambo kwa macho yake na kuwakabili viongozi wa Afrika kutoa mchango wao. Kama wengi wenu mjuavyo, tumefungua mkutano wa kuanzisha mfuko wa dunia wa kupiga vita Ukimwi,malaria na kifua kikuu kwa kukusanya zaidi ya dala bilioni 10.

Ni hapa ambapo ningependa kumshukuru Kanzela na waziri wake Heidemarie (Wieczorek-zeul)- kwa kazi njema walioifanya.“

Nae Kanzela wa Ujerumani bibi Merkel, alitaja mafanikio yaliopatikana mwishoni mwa mwaka huu chini ya uwenyekiti wa Ujerumani wa kundi la G-8 katika kulisaidia bara la Afrika.

Akaueleza ule mkutano wa kilele wa kundi hilo huko Heiligendamm,mashariki mwa Ujerumani,mkutano wa Berlin wa wafadhili kwa mfuko wa dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na malaria hapo septemba pamoja na ule mkutano wa hivi majuzi kati ya Afrika na Umoja wa Ulaya mjini Lisbon,Ureno kuwa ni hatua moja kwenda mbele.

Sasa iliobaki ni kutunga mashauri na mapendkezo kwa kipindi kijacho ambapo japan itakuwa ni mwenyekiti wa kundi hilo la G-8 ili mkondo ulioanzishwa katika kulisaidia bara la afrika usikwame:

„Tutabadilishana mawazo juu ya mkutano wa Heiligendamm ulivyopiga hatua mbele kwa bara la Afrika na kuwa hatua hiyo iliweza kuimarishwa zaidi na kikao kilichofanyika Ujerumani cha mfuko wa dunia wa kupambana na maradhi.

Muhimu kabisa kwa shabaha za mpamngo wa milenium ni vile vita dhidi ya ukimwi na maradhi mengine ya kuambukiza.

Naamini mkuatano wa kilele wa Lisbon kati ya Afrika na Ulaya ampao tulionana tena hivi karibuni ,ulitoa nao mchango mwema.

Katika mkutano wa 2006 wa Tume hii ya maendeleo ya bara la Afrika walishiriki waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tiony Blair na mwanamuziki maarufu na mkereketwa wa Afrika Bob Geldof. Tume hii shughuli zake ni kusimamia kuwa ahadi zilizotolewa kwa bara la Afrika si maneno matupu bali zinatimizwa.