1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuchel afanya mazungumzo na Hamburg

11 Aprili 2015

Kocha wa zamani wa Mainz Thomas Tuchel amekuwa akifanya mazungumzo na SC Hamburg lakini hajafikia makubaliano ya kuchukua usukani katika klabu hiyo inayokabiliwa na hatari ya kushushwa ngazi

https://p.dw.com/p/1F6MZ
Fußball Bundesliga - 1. FSV Mainz Thomas Tuchel
Picha: Getty Images

Mshauri wa Tuchel amesema hakuna mkataba uliofikiwa, kufuatia matamshi yaliyotolewa na vyombo vya habari kubwa Tuchel amekubali kusaini mktaba wa miaka minne na kuwa ataifunza Hamburg hata kama timu hiyo itaondolewa katika Bundesliga msimu huu.

Mkurugenzi wa michezo Peter Knaebel kwa sasa anaifunza Hamburg kufuatia kutimuliwa kwa Joe Zinnbauer karibu wiki mbili zilizopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohamed Dahman