1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akataa kutia saini tamko la pamoja mkutano wa G7

Sekione Kitojo
10 Juni 2018

Mkutano wa kilele wa nchi zenye utajiri wa viwanda G7 umemalizika kwa hali ya kichekesho na kitisho kipya cha vita vya kibiashara Jumamosi(09.06.2018)wakati rais Trump ghafla alipokataa kutia saini taarifa ya pamoja.

https://p.dw.com/p/2zE2r
G7 Gipfel Kanada Merkel vs Trump
Picha: Reuters/Bundesregierung/J. Denzel

Rais Trump wa Marekani  alimshambulia  kwa  kumtusi  vibaya mwenyeji  wa mkutano  huo  waziri  mkuu  wa  Canada justin Trudeau.

Dakika  chache  baada  ya  taarifa  ya  pamoja  ambayo iliidhinishwa na  viongozi wa  kundi la  washirika  saba kuchapishwa katika  mji  wa  Canada  wa  Quebec  ambao ulikuwa  mwenyeji  wa mkutano  huo, Trump  alianzisha  mashambulizi  katika  ukurasa  wa Twitter kutoka   nje  ya  nchi  hiyo  akiwa  katika  ndege  ya  rais  wa Marekani  ya  Air Force One.

G7 Gipfel Kanada Gruppenbild
Viongozi wa nchi saba zenye utajiri mkubwa wa viwanda duniani G7 mjini Quebec CanadaPicha: Reuters/ Y. Herman

Kiongozi  huyo  wa  Marekani aliondoka  mapema  kutoka  katika mkutano  huo  akiwa  njiani  kwenda Singapore katika  mkutano  wa kihistoria  wa  kinyuklia  pamoja  na  kiongozi wa  Korea  kaskazini Kim Jong Un , na  kuchukua  hatua  ya kutofautiana  na  matamshi ya  waziri  mkuu  wa  Canada  Justin Trudeau  katika  mkutano  na waandishi  habari  kabla  ya  kuondoka nchini  Canada.

"Kwa msingi  wa  matamshi yasiyo  sahihi  ya  Justin  katika mkutano  na  waandishi  habari , pamoja  na  ukweli  kwamba Canada  inatoza  ushuru  mkubwa  kwa  wakulima  wetu , wafanyakazi  na  makampuni  nchini  Marekani, nimewaagiza wawakilishi  wetu  wa  Marekani  kutoidhinisha  tamko  hilo  la pamoja  kwa  kuwa  tunaangalia  kuhusu  ushuru  katika  magari ukisababisha  kufurika  kwa  magari  ya  katika  soko  la  Marekani!. Trump  aliandika  katika  ukurasa  wa  Twitter.

"Waziri  mkuu  Justin Trudeau  wa  Canada  ameonekana  kuwa msikivu na  mtulivu  wakati tulipokutana  katika  mkutano  wa  G7 lakini  alibadilika  na  kutoa  matamshi  katika  mkutano  na waandishi  habari  baada  ya  mimi  kuondoka kwamba .. hatakubali kuburuzwa.' ni uongo na  dhaifu."

Kanada G7 Gipfel Abreise Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump akiondoka kutoka Canada akielelea SingaporePicha: Reuters/J. Ernst

Wacaanda ni wapole lakini hawataburuzwa

Hapo  mapema  Trudeau  aliwaambia  waandishi  habari  kwamba uamuzi  wa  Trump  kuweka  usalama  wa  taifa  kuhalalisha  ushuru wa  Marekani  dhidi  ya  bidhaa  zinazoingizwa  nchini  humo  za chuma  cha  pua na  bati , "ni  aina  ya  tusi" kwa  wanajeshi  wa zamani  wa  Canada  ambao  walisimama  pamoja  na  washirika wao  wa  Marekani  katika  mizozo ambayo  ni  pamoja  na  vita vikuu  vya  kwanza  vya  dunia.

"Wacanada  ni  wapole  na waelewa  lakini  pia  hatutakubali kuburuzwa,"  alisema.

G7 Gipfel in Charlevoix Kanada Trump und Macron
Rais Trump (kushoto) akipeana mkono na rais Emmanuel Macron wa UfaransaPicha: Reuters/L. Millis

Na alisema  amemwambia  Trump "itakuwa kwa  masikitiko  makubwa lakini  itakuwa  kwa  uwazi  kabisa  na  uthabiti  kwamba  tunasonga mbele  na  hatua  za  kulipiza  kisasi  ifikapo  Julai  mosi, kwa kuweka  ushuru  sawa  na  ule  ambao  Wamarekani  wamehalalisha kwa  kutuwekea."

Baada  ya  maandishi  ya  hasira  ya  Trump  katika  ukurasa  wa Twitter , ofisi  ya  waziri  mkuu  Trudeau  ilitoa  jibu fupi: "tunalenga katika  kila  kitu  tulichokamilisha  hapa  katika  mkutano  wa  G7. Waziri  mkuu  hakusema  kitu  ambacho  hajasema  kabla , katika mazungumzo  ya  wazi  na  faragha  na  rais  Trump.

Matamshi ya  hasira

Matamshi  ya  hasira  dhidi  ya  Trudeau , na  pamoja  na  kundi  la wanachama  wengine  wa  G7, ni tukio  lingine  la  hivi  karibuni ambamo Trump  amepambana  na  washirika  wa  karibu  wa Marekani, hata  wakati  akiwa  ametoa  matamshi  wa  kutia  moyo kwa  viongozi wa  kidikteta  akma  Kim  na  Vladimir  Putin  wa  Urusi.

Kanada G7 Gipfel in Charlevoix Merkel und Trudeau
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) katika mazungumzo na waziri mkuu wa Canada Justin TrudeauPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Tang

Wakati  huo huo, ahadi  ya  karibu  dola  bilioni 3 kusaidia wanawake  walioko  katika  hali  duni  na  wasichana, ikiwa  ni pamoja  na  wakimbizi kupata  elimu ilitangazwa  katika  mkutano  wa kilele  wa  G7 siku  ya  Jumamosi  nchini  Canada. Waziri  mkuu  wa Canada  Justin Trudeau , ambaye  alikuwa  mwenyeji  wa  mkutano huo  katika  mji  wa  kitalii  wa  Quebec , aliita  ahadi  hiyo "uwekezaji mkubwa  kabisa  katika  elimu  kwa   wanawake  na  wasichana walioko  katika  mizozo pia  wanaojikuta  katika  hali  ya  machafuko."

Fedha  hizo ni  zaidi  ya  kundi  la  wanaharakati  wanawake  ambalo lilikutana  na  Trudeau  pembezoni  mwa  mkutano  huo lilivyooomba, na  kusababisha   kundi  la  G7  kupata  kupongezwa  na  makundi ya kijamii na  wanaharakati, ikiwa  ni  pamoja  na  mshindi  wa  nishani ya  amani  ya  nobel  Malala Yousafzai ambaye  aliyema  fedha  hizo zitawapa  wasichana  matumaini  zaidi kwamba  wanaweza  kujenga hali  zao  za  baadaye  vizuri  zaidi."

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / dpae

Mhariri: Caro Robi