1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI:Mtoto wa Gaddafi ataka mabadiliko

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBX7

Mtoto wa kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi ametangaza mipango ya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuwa na benki kuu huru na vyombo huru vya habari.

Katika hotuba yake kupitia vyombo vya habari vya serikali mtoto huyo Sayf al-Islam Gaddafi pia ametaka kuwepo na mjadala juu ya katiba mpya ya Libya katika kuimarisha mfumo wa siasa nchini humo.

Lakini hata hivyo amesema kuwa masuala kama sheria za kiislam,musuala ya kiusalama, umoja wa taifa hilo pamoja na uongozi wa baba yake havitajadiliwa katika mjadala wowote wa kisiasa.

Mtoto huyo hana wadhifa wowote serikali, lakini baba yake kanali Gaddafi amekuwa akimuamini sana.