TRIPOLI:Matabibu waliowaambukiza watoto wa Libya HIV kujua hatma yao | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TRIPOLI:Matabibu waliowaambukiza watoto wa Libya HIV kujua hatma yao

Mahakama kuu nchini Libya itasikiliza rufaa ya mwisho ya wauguzi watano wa Bulgaria na Daktari mmoja wa Palestina wanaodaiwa kuwaambukiza kwa makusudi virusi vya HIV watoto nchini Libya.

Mahaka hiyo inatazamiwa kuunga mkono adhabu ya kifo.Hata hivyo wachanganuzi wa amasuala ya kisiasa wanasema hukumu itakayotolewa huenda ikabadilishwa kufuatia makubaliano na nchi ya Bulgaria na Umoja wa Ulaya ambapo wazazi wa watoto hao walioambukizwa virusi vya HIV watalipwa fidia.

Wauguzi hao watano wa kibulgaria na daktari ambaye amepewa uraia wa Bulgaria walikanusha mashtaka yote na kusema waliteswa ili kukiri makosa.

Kesi hii imekosolewa vikali na Umoja wa Ulaya na Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com