1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI:Kesi ya wahudumu wa afya kuahirishwa

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhu

Mahakama kuu nchini Libya inaahirisha kutolewa kwa uamuzi wa kesi inayowakabili wauguzi 5 wa Bulgaria na daktari mmoja wa KiPalestina baada ya kushtakiwa kwa kuwaambukiza watoto na virusi vya Ukimwi.Baraza Kuu la Kisheria nchini humo inasikiliza kesi hiyo tena hii leo ili kutoa uamuzi kuhusu hukumu iliyotolewa au kutoa hukumu nyepesi zaidi. Mahakama kuu ya Libya ilithibitisha hukumu ya kifo kwa wahudumu hao wa afya wiki jana.Wahudumu hao wanazuiliwa tangu mwaka 99.

Kulingana na wataalam watoto hao waliambukizwa kwasababu ya usafi duni katika hospitali waliyokuwemo mjini Benghazi.Watoto 50 kati ya hao walioambukizwa wameshakufa.

Drt Oliver Pybus wa Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza aliongoza uchunguzi huo

''Utafiti wetu unaonyesha kuwa usafi duni katika hospitali hiyo ni tatizo.Kwa miaka mingi kabla wahudumu hao kuanza kazi kwenye hospitali hiyo kulikuwa na tatizo la usafi wa vifaa na hicho huenda kikawa chanzo cha maambukizo hayo.''

Wakati huohuo pendekezo linatolewa ili kufidia jamii za watoto hao walioambukizwa.Wafanyikazi hao sita wa huduma za afya wanakana kuwaambukiza zaidi ya watoto 400 virusi vya Ukimwi na kushikilia kuwa waliungama kwasababu ya mateso.