TRIPOLI: Sarkozy amaliza ziara yake Libya
26 Julai 2007Matangazo
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amemaliza ziara yake nchini Libya. Ufaransa na Libya zimesaini mkataba wa ujenzi wa kinu cha nyuklia kwa lengo la kutengeza nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia.
Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kushirikiana katika maswala ya ulinzi.
Rais Sarkozy alikutana na rais wa Libya kanali Muamar Gaddafi mjini Tripoli na ameondoka Libya kwenda Senegal anakotarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade.