1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Makubaliano ya amani yatiwa saini

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cg

Viongozi wa makundi manne makuu ya waasi wa Chad wametia saini makubaliano ya amani pamoja na Rais Idriss Deby wa Chad katika mji wa Sirte,nchini Libya.Makubaliano hayo yametiwa saini mbele ya Rais Muammar Gaddafi wa Libya na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.Siku ya Jumamosi,Libya itakuwa mwenyeji wa majadiliano ya amani kati ya serikali ya Sudan na baadhi ya makundi ya waasi wa Darfur. Mwezi wa Novemba,Umoja wa Ulaya utapeleka vikosi vya amani kuwalinda raia na wafanyakazi wa mashirika yanayotoa misaada katika eneo la mashariki ya Chad ambalo hupakana na jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan.