TRIPOLI: Baraza kuu la mahakama kukutana Jumatatu ijayo
11 Julai 2007Matangazo
Baraza kuu la mahakama nchini Libya litakutana Jumatatu wiki ijayo kuamua ikiwa liidhinishe, libatilishe au lifutilie mbali hukumu ya kifo dhidi ya wauguzi watano wa Bulgaria na daktari mmoja wa Palestina.
Kesi ya wataalmu hao wa afya itajadiliwa na baraza hilo baada ya mahakama kuu ya Algeria kuidhinisha hukumu ya kifo dhidi yao hii leo.
Wataalamu hao walishtakiwa kwa kuwaambukiza ukimwi watoto zaidi ya 400 katika hospitali moja mjini Bengazi nchini Libya mnamo mwaka wa 1998.
Kufikia sasa watoto 56 kati ya watoto 438 walioambukizwa ukimwi wamefariki dunia.
Umoja wa Ulaya umetaka wataalamu hao wasamehewe.