TP Mazembe yaingia fainali ya klabu bingwa ya dunia | Michezo | DW | 15.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

TP Mazembe yaingia fainali ya klabu bingwa ya dunia

Imeishangaza Internacional ya Brazil kwa ushindi safi wa mabao 2-0

Timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa timu ya kwanza barani Afrika kuingia fainali za klabu bingwa ya dunia, kwa kuicharaza mabingwa wa Copa Libertadores, Internacional ya Brazil, mabao 2-0 jana usiku huko Abu Dhabi.

Mulota Kabangu alifunga bao la kwanza la Mazembe dakika ya 53 ya mchunao huo na baadaye Dioko Kaluyituka akaongeza la pili dakika ya 85, muda mfupi kabla kipyenga cha mwisho kupulizwa.

TP Mazembe ambayo ni mabingwa wa Afrika, sasa itavaana na mshindi wa mchuano wa leo kati ya mabingwa wa Ulaya, Inter Milan ya Italia na mabingwa wa barani Asia, Seongnam Iihwa, ya Korea Kusini, kwenye fainali itakayochezwa Jumamosi wiki hii.

 • Tarehe 15.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QZP9
 • Tarehe 15.12.2010
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/QZP9