1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOULOUSE:Uongozi wa Kampuni ya Airbus kujadiliwa

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiD

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anakutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel hii leo kuafikiana kuhusu uongozi wa kampuni inayotengeza ndege aina ya Airbus,EADS.Kampuni hiyo inayosimamiwa na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani inazongwa na matatizo ya uongozi.

Kabla ya mkutano huo ,kwa mujibu wa Bi Merkel masuala ya biashara sharti yawe mstari wa mbele ili kulinda maslahi ya kampuni ya EADS.Bi Merkel aliyasema hayo alipozungumza na gazeti la kila siku la Handelsblatt.

Viongozi hao wawili wa nchi wanakutana kwenye makao makuu ya kampuni ya Airbus yaliyoko mjini Toulouse kabla kukutana na washika dau aidha kuzuru kiwanda kimoja.Rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy na Bi Angela Merkel wanakutana na waandishi wa habari ifikapo saa sita za mchana.

Kampuni ya Airbus inapendekeza mabadiliko makubwa ili kutafuta suluhu ya utata uliosababishwa na msukosuko wa mpangilio na biashara.Matatizo hayo yalisababisha hasara japo kampuni hiyo iliunda ndege nyingi mwaka jana hususan ndege aina ya Airbus A380 Superjumbo inayotarajiwa kuanza kazi baadaye mwaka huu.