TORONTO:Canada yamfurusha balozi wa Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 30.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TORONTO:Canada yamfurusha balozi wa Sudan

Serikali ya Canada imeamua kumfurusha mwanadiplomasia wa Sudan nchini humo kama njia ya kulipiza kisasi baada ya Sudan kumtimua mwakilishi wa nchi hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Canada imesema uamuzi wake utaanza kutekelezwa Septemba mosi na tayari mwanadiplomasia huyo wa Sudan nchini Canada ameshajulishwa kuhusu hatua hiyo.

Canada imechukua uamuzi huu siku chache baada ya Sudan kutangaza kuwatimua balozi wa nchi hiyo na mjumbe wa Umoja wa Ulaya nchini mwake kwa madai ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa upinzani wa Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com