TOKYO:Mabadilko ya baraza la mawaziri kufanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 27.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO:Mabadilko ya baraza la mawaziri kufanyika

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amejiandaa kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri hii leo ili kuijenga upya serikali yake kufuatia kushindwa vibaya kwa chama chake katika uchaguzi.

Bwana Abe anatarajiwa kuwateua mawaziri ambao hawana dosari ya kuhusika na kashfa yoyote zoezi ambalo linatarajiwa kuchunguzwa kwa makini kufuatia shutuma kwamba bwana Abe aliwa chagua rafiki zake kuwa mawaziri kwenye baraza la mawaziri la sasa.

Baraza hilo la sasa litajiuzulu mchana wa leo na kuchaguliwa jipya.

Aidha Waziri mkuu Abe anatarajiwa asubuhi hii kuwateua viongozi watatu wa chama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com